Breaking News

BREAKING: Nyalandu kuanza kuchunguzwa, Dr. Kigwangalla awaagiza Polisi na TAKUKURU

on

Ni habari kutoka Bungeni Dodoma leo November 13 2017 na ni agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Hamisi Kigwangallah dhidi ya aliyekua Waziri wa Maliasili awamu iliyopita Lazaro Nyalandu.

Dr Kigwangalla ameliagiza Jeshi la Polisi na TAKUKURU kuanza mara moja kumchunguza aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kufuatia tuhuma mbalimbali zinazomkabiliĀ za matumizi mabaya ya madaraka.

Agizo hili limetolewa wiki mbili baada ya Lazaro Nyalandu kutangaza kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya CCM ikiwemo Ubunge wa Singida Kaskazini.

BARUA YA KATIBU MKUU WA CCM KUHUSU KUJIUZULU KWA NYALANDU, “TULISHAANZA KUMCHUKULIA HATUA”

Soma na hizi

Tupia Comments