Mix

Uteuzi mwingine alioufanya Rais John Magufuli leo May 30 2016

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa Serikali ambapo amemteua Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani. Kabla ya uteuzi huo Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi, uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Uteuzi wa Anne Semamba Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo. 

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es salaam Institute of Technology – DIT). 

Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake, uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

ULIKOSA ALICHOKIONGEA MBUNGE JOSHUA NASSARI BAADA YA BUNGE KUKATAA KUJADILI WANAFUNZI KUFUKUZWA CHUO? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI  

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments