Michezo

Man City na Man United wametoka sare yao ya 52 leo

on

Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 imeendelea usiku wa leo April 27 kwa mchezo mmoja wa Ligi Kuu England kuchezwa katika uwanja wa Etihad jijini Manchester.

Mchezo wa EPL leo ulikuwa unazikutanisha timu mahasimu kutoka jiji la Manchester kati ya Man United waliyowafuata Man City katika uwanja wao wa Etihad kucheza mchezo wao wa 33 wa Ligi Kuu England.

Mvuto na upinzani wa Manchester Derby umeongezeka kutokana na upinzani wa kocha Jose Mourinho wa Man United na kocha Pep Guardiola wa Man City ambao walitoka nao toka LaLiga mmoja akiwa anaifundisha Barcelona na Mourinho akiifundisha Real Madrid.

Mourinho na Guardiola leo wamelazimisha sare (0-0) ya 7 toka waanze kukutana katika michezo yao 19 Mourinho akiwa ameshinda mara 4 na kupoteza mara 8 lakini Man City leo wanatoka sare yao ya 52 dhidi ya Man United katika mara zao 174 walizowahi kukutana wakiwa wamepoteza mara 72.

Soma na hizi

Tupia Comments