Top Stories

Mbunge wa zamani wa Dimani ZNZ afikishwa Mahakama ya Kisutu

on

Leo July 12, 2018 Aliyekuwa Mbunge wa Dimani Zanzibar, Abdalah Sharia Amer, na mwenzake wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya kutapeli Shilingi Milioni 55.

Mbali ya mbunge huyo mshtakiwa mwingine ni Dk.Athumani Rajabu.

Akiwasomea hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Janet Magoho amedai mbele ya Hakimu Mkazi Hamisi Ally kuwa, washtakiwa wametenda kosa hilo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kati ya July 17 na September 29 2017 ndani ya Jiji la DSM.

Imedaiwa, siku hiyo washtakiwa hao kwa pamoja na kwa kudanganya walijipatia kutoka kwa Dr. Abdi Hirsi Warsame kiasi cha Shilingi Milioni 55 kwa kumdanganya kuwa wangemsambazia vifaa tiba vya hospitality huku wakijua kuwa siyo kweli.

Hata hivyo, washtakiwa wote, wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo wametakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya sh. Milioni 27.5 kila mmoja.

Pia ametakiwa kuwasilisha fesha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni 27.5 au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirisha hadi July 12 (kesho) kwa ajili ya dhamana.

BREAKING LIVE: CHADEMA waweka wazi wagombea wake, wakana wagombea feki

Soma na hizi

Tupia Comments