Habari za Mastaa

Sio siri tena Ommy Dimpoz kaamua kuweka hadharani

on

Leo June 6,2019 mwimbaji kutokea kwenye industry ya Bongo Fleva Ommy Dimpoz amechukua headlines tena kwenye mitandao ya kijamii baada ya kupost picha pamoja na videos zikimuonyesha akiwa na mtoto mdogo na wengi kuhisi labda ni mtoto wake.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Ommy Dimpoz ameandika caption ambayo wengi wameipigia mstari na kusema kuwa inawezekana yule ni mtoto wake, Ommy hakutaja jina la mtoto huyo lakini alionekana akiwa nae Aiport ya Barcelona kama wanasafiri nae hivi.

Ommy Dimpoz ni miongoni mwa mastaa ambao hawapendi kuweka mambo yao hadharani ingawa ni mtu wa kupost picha mara kadhaa kupitia ukurasa wake wa instagram, hivyo inasemekana huyo ni mtoto wake kutokana na staa huyo kutumia picha na video akiwa na mtoto kudai kuwa ndio sababu inayomfanya aende sana Ulaya.

Ommy Dimpoz amempost mtoto huyo akiwa nae na kuandika hivi “Vipi Dengue Imeisha Nirudi nae? Haya Nafikiri yale Maswali ya unafanya nini Ulaya kila siku YAMEISHA😁😁” ameandika Ommy Dimpoz kupitia ukurasa wake wa Instagram.

VIDEO: NOMA!! NANDY NA WILLY PAUL WALIVYO PEWA SHANGWE SUMBAWANGA

Soma na hizi

Tupia Comments