January 3, 2018 Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma imeshindwa kufikia lengo la kukusanya mapato ya Shilingi Milioni 200.8 kwa mwezi kutokana na utendaji mbovu wa Watendaji wa Manispaa hiyo kushindwa kusimamia vyema ukusanyaji huo.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mkoani Kigoma Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mwailwa Pangani amesema licha ya Manispaa hiyo kushindwa kufikia lengo hilo lakini kila mwezi mapato yamekuwa yakiongezeka na hivyo kuahidi kufikia lengo hilo hivi karibuni.
LIVE MAGAZETI: Inasikitisha mazishi ya aliekufa akifunga ndoa, CHADEMA yaibuka na mapya