Premier Bet
TMDA Ad

Top Stories

Polisi nchini Uganda waomba radhi kwa Mwandishi wa Habari kupigwa

on

 Taarifa kutoka Jeshi la Polisi nchini Uganda ni kuwa limeomba radhi baada ya Askari wake kuonekana kwenye video iliyosambaa mitandaoni wakimpiga Waandishi wa habari aliyekuwa akitekeleza majukumu yake.

Mwandishi huyo alikuwa akiripoti matukio wakati wa maandamano ya Wananchi waliokuwa wakipinga kushikiliwa kwa Mbunge, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine.

Polisi Uganda wameeleza kuwa kitendo hicho kilichofanywa na Askari wake si cha weledi na kuongeza kuwa wahusika watakamatwa kwa mujibu wa Sheria.

Video ikionesha Askari wakimpiga vibaya Mwandishi wa Shirika la Reuters, James Akena imesambaa katika mitandao ya kijamii na kuzua hasira za watetezi wa haki za binadamu.

Viongozi Maarufu waliomzika Dada yake Rais Magufuli “Kikwete, Mwinyi, Mkapa, Odinga” na wengine (+video)

Soma na hizi

Tupia Comments