Aliyekuwa mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama amemshambulia kwa maneno rais wa Marekani Donald Trump kwa kumwambia kuwa mapungufu yake yameleta machafuko nchini humo tangu kuingia kwake madarakani mwaka 2016.
Michelle anaamini kuwa mgombea urais kupitia Chama Cha ‘Democratic’ Joe Biden atarejesha amani , afya na ustawi nchini humo.