Michezo

Ronaldo anajikubali, kataja goli lake bora maisha yake ya soka

on

Staa wa soka wa club ya Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo ameendelea kujimwagia sifa kuhusiana na goli lake alilowafunga Juventus wakati akiwa Real Madrid kuwa ndio goli lake bora la muda wote ya maisha yake ya soka.

Ronaldo ameweka wazi kuwa amejaribu mara nyingi kutaka kupiga au kufunga kama alivyolifunga goli hilo ambalo ndio anaamimi kuwa bora katika maisha yake ya soka lakini inashindikana.

“Goli langu ninalolipenda ni lile nililowafunga Juventus, hata hivyo ni goli langu bora nililowahi kufunga katika maisha yangu ya soka, nimejaribu mara nyingi kutaka kufunga vile lakini sikufanikiwa, nafikiri sitakuja kuona goli ( bicycle goal) kama hilo tena”

“Yamkini ni goli bora nililowahi kuliona hata kama mwingine akitokea akawahi kufunga kama hilo lakini hili ni bora”

Soma na hizi

Tupia Comments