Habari za Mastaa

Ushauri wa Bill Nass kwa Roma Mkatoliki na wenzake

on

Kupitia kipindi cha The Weekend Chart Show April 14, 2017 kinachorushwa na Clouds TV rapa Bill Nass ambaye anatamba na hit song ya Mazoea amemuasa Roma Mkatoliki na wenzie ambao walikumbwa na mkasa wa kutekwa.

Bill Nass amewataka Roma na wenzie kuendelea na maisha kwa kufanya kazi ingawa hawatokuwa vizuri lakini kwa sababu wana uhai na uzima katika maisha yao wanapaswa kumshukuru Mungu.

>>>”Wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwa wako hai. Wendelee kufanya kazi kwa moyo, japo unapokuwa na pressure huwezi kufanya. Kwa mfano, mimi tu nikiwa hivyo mood za studio zinakata. Japo wao wanaweza kuwa zaidi ya hapo, ila hizo ni changamoto tu, so, isiwafanye wakaishia hapo as long as wako hai na wazima.” – Billnass.

VIDEO: “Naogopa kupanda ndege” – Nikki wa Pili

Soma na hizi

Tupia Comments