Mix

EXCLUSIVE: Watanzania wagundua dawa ya wizi wa magari (+video)

on

Ikiwa ni Machi 5, 2019 tunayo Exclusive stori kutokea kwa vijana wa Kitanzania waliogundua mfumo maalum wa kudhibiti wizi wa magari kwa kutumia simu ya kiganjani.

Saleh Ally ni kiongozi wa kundi la vijana watano waliofanya ugunduzi huo kutokea maeneo ya Kagera Dar es Salaam, ambapo anasema hadi sasa wameshafunga mfumo huo katika magari 200, huku wakiwa wameanza miaka mitatu iliyopita.

Anasema kuwa mtu aliyeunganishwa na mfumo huo anapatiwa namba maalum ambapo anaweza kuzima ama kuliwasha gari lake kwa kutumia simu, pia endapo kama limeguswa simu itajipiga kuashiria kuna jambo linaendelea katika gari lako.

Mfumo huu ni offline kwa maana sio lazima uwe na simu ya Smartphone ama internet bali ni simu ya aina yoyote, pia unaweza kuliona gari lako lilipo moja kwa moja kupitia mfumo wa video,“amesema.

SIMANZI: MWILI WA BOSS RUGE UKIWEKWA NDANI YA KABURI KIJIJINI KWAO

Soma na hizi

Tupia Comments