Maafisa watano wa polisi wa Kenya walifikishwa mahakamani siku ya Jumatano, wakishukiwa kumsaidia mwanamume anayedaiwa kuwaua makumi ya wanawake kutoroka katika seli ya polisi Nairobi.
Polisi walianzisha msako siku ya Jumanne baada ya anayedaiwa kuwa muuaji wa mfululizo Collins Jumaisi na Waeritrea 12 kuzuka kutoka kituo cha polisi katika eneo la soko kuu la mji mkuu wa Kenya.
Jumaisi, 33, aliyeelezewa na polisi kama “vampire, psychopath,” alikamatwa mwezi uliopita baada ya ugunduzi wa kutisha wa miili kadhaa iliyokatwakatwa katika eneo la kutupa taka katika eneo la makazi duni katika mji mkuu wa Kenya.
Yeye na wafungwa wengine walionekana kutoroka kwa kukata paa la matundu ya waya katika kituo hicho.