Marekani imetangaza vizuizi vya Viza dhidi ya Maafisa wa Ethiopia na Eritrea wanaoshukiwa kwa vita katika Mkoa wa Tigray, ikisema waliohusika hawakuchukua hatua stahiki kumaliza uhasama.
Maelfu waliuawa na wengine kulazimika kukimbia makazi yao tangu Novemba baada ya Waziri Mkuu, Abiy Ahmed kutuma Vikosi kukamata na kudhibiti Viongozi wa Chama Tawala Mkoani humo, TPLF.
Marekani imesema Wananchi wa Tigray wanaendelea kuteseka na ukiukwaji wa Haki za Binadamu na wanahitaji msaada wa kibinadamu ambao unazuiwa na Majeshi ya Ethiopia na Eritrea.
MDOGO WA JIMMSON ASIMULIA AIBUKA MAPYA MAJAMBAZI WALIVYOMVAMIA KAKA YAKE, “DAMU ILIMUISHIA”