Maafisa wa Wizara ya Katiba na Sheria wnatarajia kuwafikia Wananchi wenye Changamoto mbalimbali kwa lengo la kutatua Migogoro mbalimbali ikiwemo migogoro sugu ya Ardhi , Mirathi , Migogoro ya mipaka kwenye maeneo ya uchimbaji huku wananchi wakitakiwa kujitokeza kwa wingi na kutoa ushirikiano kwa Maafisa hao.
Akizungumza Mara baada ya kufungua warsha hiyo iliyowakutanisha Maafisa Mbalimbali ndani ya Mkoa wa Geita Katibu Tawala Mkoa wa Geita , Mohamed Gombati amesema kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia inalenga kuwafikia watu ambao wameshindwa kupata utatuzi wa kisheria katika Migogoro.
“Matarajio ni nini , kubwa kuliko yote ni kuhakikisha tunawafikia wananchi ambao walipaswa kupata huduma hizi tutapunguza gharama lakini tutapunguza Muda kwa kuwafikia wananchi wetu tunao wajibu wa kuwafikia wananchi na kuwapa elimu kuhusu Masuala ya kisheria , ” Katibu Tawala Mkoa wa Geita Mohamed Gombati.
Candird Nasua ni Wakili wa serikali kutoka wizara ya Katiba na Sheria amesema lengo la Kampeni hiyo ni kuwafikia wananchi wote wenye uhitaji ambapo katika Halmashauri zote za Mkoa wanatarajia kutembelea kila kata kumi ambapo watatoa msaada wa kisheria ikiwemo elimu.
” Kampeni hii inatokana na sheria ya huduma za msaada wa kisheria sura ya 21 ambayo ni ya mwaka 2021 na hii inatokana na inahitaji kubwa la wananchi kupata huduma za kisheria wako wananchi ambao hawana uwezo kwa kumudu gharama za Mawakili lakini pia wako wananchi ambao wako mbali na maeneo ya mijini tunaweza kusema wale ambao hawawezi kufikika kwa urahisi , ” Wakili wa Serikali Wizara ya katiba na Sheria , Candird Nasua.
Mmoja washiriki katika warsha hiyo kutoka Dawati la Jinsia na watoto Polisi Geita SGT. Rebecca Manase amesema elimu hiyo ambayo wameipata itaenda kuisaidia Jamii ambayo haina Msaada wa elimu ya kisheria huku akisema matukio mengi ya ukatili yanachangiwa na Migogoro ya Kifamilia.
“Katika elimu ambayo tunaenda kuipata kuhusiana na Masuala ya kisheria kuelekea hii wiki ya sheria kwa watu walioko pembezoni mwa mji wa Geita ni bora zaidia na tunaweza kupata anasa kubwa katika maeneo mbalimbali na watu ambao wanapata elimu ndani ya maeneo karibu na Mahakama zetu au huduma zetu za Dawati la Jinsia , Polisi kutoka Dawati la Jinsia Geita , SGT. Rebecca Manase.