Wafanyabishara wa Soko Matola Jijini Mbeya wamelalakia Kutokuwepo kwa uongozi rasmi katika Soko hilo
Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya alipotembelea Soko hilo kwa lengo la Kusikiliza na kutatua kero za Wafanyabishara hao wamesema kwa muda mrefu soko hilo limekosa Viongozi sahihi watakao waongoza na badala yake Viongozi waliokuwepo hawapo kisheria kwa maana hawakuchaguliwa na Wafanyabishara.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa amejibia Suala hilo na kuagiza ufanyike uchaguzi ndani ya mwezi mmoja ili wapatikane Viongozi watakaoweza kutetea maslahi ya Wafanyabishara hao .
Malisa amefanya ziara hiyo akianzia kata ya Iziwa ambapo alikagua shule ya Sekandari Iziwa na Kufanya mkutano wa Hadhara.