Top Stories

Maagizo ya DC Sabaya kwa Maafisa Utumishi “nawapa siku 3” (+video)

on

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ametoa siku tatu kwa Idara ya Utumishi kutoa maelezo ya sababu za kutopeleka Nyaraka Muhimu za Walimu waliostaafu kwa zaidi ya miaka miwili kwa Katibu Mkuu wa Hazina.

Sabaya ameitaja hatua hiyo ya Idara ya Utumishi kama hatua ya kuichonganisha Serikali na Watumishi wake kwa kuwa Serikali isingekosa hela za kuwalipa wastaafu hao.

Sabaya amesema, baada ya siku tatu Walimu wote waandikiwe barua na Utumishi kuthibitisha madeni na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya itafanya mawasiliano na hazina kufikisha nyaraka zote za muhimu ili Walimu hao wapate stahiki.

Soma na hizi

Tupia Comments