Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Maagizo ya Kairuki kwa Bodi ya UDART
Share
Notification Show More
Latest News
Jorginho aondoka Chelsea na kusaini Arsenal
February 1, 2023
Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain
January 31, 2023
Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza
January 31, 2023
Waliokutwa na meno ya tembo wahukumiwa miaka 20 jela (+video)
January 31, 2023
Maji ya ajabu yanayotoka bombani Johannesburg
January 31, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > Maagizo ya Kairuki kwa Bodi ya UDART
Top Stories

Maagizo ya Kairuki kwa Bodi ya UDART

November 16, 2022
Share
4 Min Read
SHARE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa,(OR-Tamisemi) Mhe. Angellah Kairuki ameitaka Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa DART kuhakikisha inafanya kazi kwa bidii katika kubuni mikakati ya kuboresha zaidi huduma ya usafiri ndani ya Jiji la Dar es Salaam na ikiwezekana kuchukua hatua za kuanzisha huduma hiyo katika majiji mengine nchini.

Wito huo ameutoa leo Novemba 15,2022 Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa DART na kusema uanzishaji wa chombo hicho cha Serikali chini ya usimamizi wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ni muhimu kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya nchi kijamii na kiuchumi.

Aidha, amesema chombo hicho kina wajibu wa kuhakikisha kinasimamia utekelezaji na uendeshaji wa Mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka katika Jiji la Dar es salaam ili azma ya Serikali katika uanzishaji wake iweze kutimia.

Amesema kutokana na usimamizi imara unaofanywa na DART chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI katika kutekeleza mradi wa DART, Jiji la Dar es Salaam limefanya uamuzi thabiti wa kutoa huduma hii ya usafiri katika ubora wa kiwango cha kimataifa.

“TAMISEMI inaendelea na hatua za utunzi wa Sheria ya Usafiri wa Umma Mijini ambapo pamoja na mambo mengine, kupitia Sheria hiyo inapendekezwa kuanzisha chombo chenye mamlaka ya kutekeleza majukumu yake kihuduma, kibiashara (kwa kushirikiana na sekta binafsi) na kwa uharaka zaidi katika kuwafikia wananchi kwa huduma ya usafiri wa umma na kuondokana na utegemezi wa ruzuku ya Serikali”. Amesema Waziri Kairuki.

Pamoja na hayo amesema kutokana na kazi zinzoendelea katika ujenzi wa miundombinu Awamu ya Pili kwa barabara iendayo Mbagala Rangitatu, na huduma ya mabasi inayoendelea Awamu ya Kwanza katika Barabara ya Morogoro na maeneo mengine kama vile Hospitali ya Mloganzila na Kibaha (Mkoa wa Pwani) , ni dhahiri kuwa DART, inatakiwa kujipanga kupambana na changamoto za usafiri wa umma zitakazoongezeka katika jiji la Dar es Salaam.

Amesema ongezeko la idadi ya watu katika Jiji la Dar es Salaam kwa mwongo uliopita limekuwa kubwa zaidi kuliko kasi ya uboreshaji wa miundombinu na hivyo kwa kiwango kikubwa kuongeza msongamano wa magari barabarani. Jiji la Dar es Salaam.

Nae Mwanyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara, Dkt. Florens Turuka amesema Bodi itahakikisha inakuwa bega kwa bega na uongozi wa menejimenti ya Wakala  kusaidia utekelezaji wa mikakati ya utekelezwaji wa program zote zilizopo na zinazoendelea ili zikamilike kwa wakati.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka-DART, Dkt. Edwin Mhede amesema Ujenzi wa miundombinu ya awamu ya pili ya Mradi wa DART unatekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 141.71.

Amesema Serikali imelipa fidia ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 30.25 kwa wananchi wapatao 92 ambao maeneo yao yaliathiriwa na utekelezaji wa mradi huu katika mitaa ya Mianzini (Mbagala), kwa Azizi Ally, Misheni na Chang’ombe.

Pamoja na hayo amesema Wakala unaendelea kukamilisha zabuni ya kununua mabasi 177 ili kuweza kukamilisha idadi ya mabasi  387 kulingana na usanifu, ili kukamilisha awamu ya kwanza kuweza kutoa huduma kamili kikamilifu.

You Might Also Like

Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain

Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza

Waliokutwa na meno ya tembo wahukumiwa miaka 20 jela (+video)

Maji ya ajabu yanayotoka bombani Johannesburg

Biden akataa kutuma ndege za kivita Ukraine

TAGGED: TZA HABARI
Pascal Mwakyoma TZA November 16, 2022
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo November 16, 2022
Next Article Donald Trump aibuka na kusema “Nitagombea Urais 2024”
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Jorginho aondoka Chelsea na kusaini Arsenal
Sports February 1, 2023
Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain
Top Stories January 31, 2023
Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza
Top Stories January 31, 2023
Waliokutwa na meno ya tembo wahukumiwa miaka 20 jela (+video)
Top Stories January 31, 2023

You Might also Like

Top Stories

Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain

January 31, 2023
Top Stories

Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza

January 31, 2023
Top Stories

Maji ya ajabu yanayotoka bombani Johannesburg

January 31, 2023
Top Stories

Biden akataa kutuma ndege za kivita Ukraine

January 31, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?