Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Edwin Rutageruka amewataka Wadau wa Alizeti wa Mkoa wa Singida kupanga mikakati ya pamoja ya kuongeza uzalishaji wa Alizeti ili kutosheleza mahitaji makubwa ya viwanda vya kusindika alizeti ambavyo vinashindwa kuzalisha mafuta kwa mwaka mzima kutokana na kukosekana kwa malighafi.
Rutageruka ametoa wito huo wakati akiongea na Wasindikaji, wakulima wa alizeti na watendaji wa Serikali wakati wa Mkutano na Wadau wa alizeti wa Mkoa wa Singida.
Mkutano huo umeandaliwa na TANTRADE kwa ushirikiano na Uongozi wa Mkoa wa Singida pamoja na Chama cha Wasindikaji wa Mafuta ya Alizeti Singida ( SISUPA) na kushirikisha Wadau wapatao 110 kutoka Mkoa wa Singida.