Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa yaliyopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam.
Ametoa agizo hilo leo alipotembelea mradi wa machinjio ya kisasa yaliyopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa mpaka sasa asilimia 95 ya ujenzi wa mradi huo imekamilika ikiwemo mitambo ya kuchinjia na eneo la maji taka wakati tangi la kuhifadhia maji, chumba baridi cha kuhifadhia nyama na kuweka sakafu eneo la nje ya kiwanda ambapo mpaka kufikia Juni 30, 2021 kazi zote zitakuwa zimekamilika.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa jiji la Dar es Salaam kuhakikisha mifereji ya maji taka yanayotoka katika machinjio hayo yaelekezwe kwenye mifereji maalum hadi mtoni ili yasiingie kwenye makazi ya watu .
Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa ni vyema wafanyabiashara wakaanza kutumia machinjio hayo ya kisasa na yeyote anayetaka kutumia aruhusiwe “mitambo ipo tayari, ni vyema tukawazoesha ili muweze kujua taratibu, mwenyekiti unaweza kuwa unaandaa baadhi ya ng’ombe wakawa wanakuja kwenye machinjio mapya.
Waziri Mkuu pia amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha anakamilisha haraka taratibu za ujenzi wa sehemu ya reli inayoingia katika machinjio hayo kwa ajili ya kushusha ng’ombe.
Akizungumzia ujenzi wa mradi huo ambao umefikia asilimia 95, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Jumanne Shauri amesema mradi utagharimu Sh bilioni 12.49 utakapokamilika na utasaidia kupanua wigo wa masoko ya nje na kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na ng’ombe na mbuzi.