Mix

‘Hata nitakapotangulia mbele ya haki niiache Tanzania ikiwa na amani’ -Rais JPM

on

July 25 2016 Serikali ya Tanzania imefanya  maadhimisho ya siku ya mashujaa ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais John Pombe Magufuli alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yaloiyofanyika kitaifa Dodoma.

Katika hotuba yake Rais Magufuli hakuacha kusisitizia suala la amani katika taifa huku akiwataka watanzania wote kwa pamoja kuhakikisha wanailinda na kuidumisha.

Tunapoadhimisha siku ya mashujaa, tunawakumbuka wote waliotoa uhai wao kuhakikisha nchi inakuwa na amani, hawa mashujaa wetu waliofariki hawakujali dini, vyama wala makabila yao, tunapowakumbuka tuilinde amani‘ –Rais Magufuli

Niviombe vyama vyote wawe wahubiri wa amani kwakuwa  maendeleo ya nchi yetu yatapatikana kama tutailinda amani tuliyonayo, hata nitakapotangulia mbele ya haki niiache Tanzania ikiwa na amani’ –Rais Magufuli

Lakini pia Rais Magufuli hakulikalia kimya hili la mpango wa Serikali kuhamishia makazi yake Dodoma ambapo amesema …>>>’Haiwezekani Serikali ninayoiyongoza ishindwe kuhamia Dodoma, leo tunamkumbuka pia baba wa taifa aliyesema makao makuu yawe Dodoma, sisi hatuwezi kupinga hatua hiyo‘ –Rais Magufuli

ULIIKOSA HII NI KWELI RAIS MAGUFULI ANAKATAA USHAURI? MZEE MAKAMBA KAFUNGUKA

Soma na hizi

Tupia Comments