Maajabu

VIDEO: Maajabu mengine ya jiji la Dar, mwanamke adaiwa kufa kisha kufufuka

on

Asubuhi ya April 18, 2017 kulisambaa taarifa za kufufuka kwa mwanamke ambaye alidaiwa kufa baada ya kugongwa na gari usiku wa kuamkia leo na kuthibitshwa kifo chake.

Mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Anna mkazi wa Tanki Bovu jijini Dar es Salaam anadaiwa kugongwa na gari usiku wa April 17, 2017 siku ya Pasaka kisha kufanyiwa vipimo na kuthibitika kuwa kweli amefariki, lakini taarifa za kifo hicho ziliposambaa ndipo zikaibuka taarifa nyingine kuwa angali hai.

Katika hali ya kustaajabisha, vijana wawili waishio mtaa mmoja na mwanamke huyo walijitokeza na kudai kuwa mwanamke huyo hakufa bali yupo hai amechukuliwa kimazingara.

AyoTV na millardayo.com imewapata vijana hao ambao wamefanikisha kurudishwa kwa mwanamke huyo na hapa wanasimulia mlolongo mzima…

Bonyeza play kutazama…

VIDEO: Mwongozo uliotolewa Bungeni baada ya mauaji ya Askari 8. Bonyeza play kutazama.

Soma na hizi

Tupia Comments