Top Stories

Maajabu atumia Bilioni 5 ajibadili awe kama paka amfurahishe mumewe (+video)

on

Mwanamke mmoja ambaye ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii Jocelyn Wildenstein, anatajwa na Kitabu cha Kumbukumbu za Dunia kuwa enzi za ujana wake alifanya upasuaji katika uso wake uliomgharimu kiasi cha shilingi bilioni 5 za Kitanzania ili tu afanane na mnyama paka kisha amfurahishe mumewe.

Jocelyn Wildenstein ambaye ni maarufu kwa jina la Catwomen, mwenye uraia wa nchini Marekani alifanya upasuaji wa sura mara 24 akijaribu kutengeneza uso wake ufanane na wa paka.

Jocelyn alifanya yote hayo kujaribu kumfurahisha mumewe, Bilionea Alec Wildenstein aliyekuwa na mapenzi mkubwa kwa paka.

Kwa kumtazama usoni, Jocelyn amebadilika na muonekano wa sura yake haupo kama binadamu wa kawaida. Hali hiyo ndiyo iliyomfanya ajulikane kama Catwomen.

Pamoja na kufanya uamuzi huo wa hatari, mwaka 1999 ndoa yao ilivunjika rasmi na Alec akaoa mwananmke mwingine.

Soma na hizi

Tupia Comments