Kampuni ya Apple kutoka nchini Marekani imezindua kifaa kipya cha kuvaa machoni kilichopewa jina la Apple Vision Pro ambacho kitamsaidia Mtu kuutazama ulimwengu na maeneo yake mbalimbali kwa uhalisia ikiwa
ni kidigitali zaidi.
Kifaa hiki kinatumia mfumo wa 3D, na unaweza kukifanya kifanye kazi kwa kutumia mkono, macho pamoja na sauti huku kikikuwezesha kuingia mitandaoni na kuperuzi vitu mbalimbali kwa teknolojia ya kisasa zaidi.
Moja ya vitu vimefanya kifaa hiki kizungumziwe sana ni kuhusu gharama yake kwani ili uweze kukimiliki kifaa hiki unatakiwa kutoa takribani USD $3499, sawa na zaidi ya milioni Tsh. 8… leo @AyoTV_ imeongea na Samweli Masika, Mtaalamu wa Teknolojia kutoka Tasisi ya Inauzwa hapa Dar
es Salaam ili kujua zaidi jinsi kifaa hiki kinavyofanya kazi.
Wale Wakali wa kwenda na kila matoleo ya kidigitali vipi Apple Vision Pro mtaichangamkia kwa Tsh.milioni 8+ ?.