Leo na kuletea simulizi fupi ya Paul Richard Alexander ambaye ni Mwanasheria, Mwandishi wa Vitabu kutoka nchini Marekani ambaye alizaliwa Mwaka 1946 na miaka sita mbele Mwaka 1952 alipata ugonjwa wa Polio uliomfanya apooze kuanzia shingoni hadi miguuni na kufanya maisha yake yote tangu wakati huo kuwa ni ya kulala tu kwenye mashine Maalum inayomsaidia kupumua na kuendelea kuishi ambayo inaitwa Mapafu ya Chuma (Iron Lung au Tank Ventilator.
Tatizo lilianzia wakati wa Ugonjwa wa Polio miaka ya 1950s ambapo Watoto wengi wa Dallas, Texas akiwemo Alexander walipelekwa Parkland Hospital na kutibiwa kwenye iron lungs, Hiyo haikumkatisha tamaa alianza kusoma kwa Walimu kumfuata nyumbani hadi akahitimu W.W. Samuel High Mwaka 1967 bila kwenda Darasani baadaye alipata Scholarship Southern Methodist University na akahamishiwa Chuo Kikuu cha Texas, Austin ambako alipata Degree yake ya kwanza mwaka 1978 kisha Degree ya Sheria Mwaka 1984 na akapata kazi ya kufundisha Sheria kisha baadaye akaanza shughuli za Uwakili Mwaka 1986.
Ameandika kitabu cha kumbukumbu ya maisha yake kinachoitwa “Three Minutes For A Dog, April 2020 ambacho alitumia miaka 8 kukikamilisha akitumia fimbo ya plastic aliyoweka mdomon na peni kuandika story kwenye keyboard au wakati mwingine alikuwa anampa vitu vya kuandika Rafiki yake na akawa anamsaidia.
R KELLY AKUTWA NA HATIA “ANAWEZA KUFUNGWA HADI KIFUNGO CHA MIAKA 10 JELA”