Top Stories

Maalim Seif akiri kupokea barua kutoka Serikali ya Mwinyi, ajibu

on

Aliyekuwa Mgombea wa Urais Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo  Maalimu Seif amesema wamepokea barua kutoka serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu jina la Makamu wa Rais na wanafanyia kazi .

Maalim Seif aliendelea kusema kwamba chama cha ACT Wazalendo bado hakijaamua kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kimataifa (SUK).

Aidha aliongezea “chama bado tunashauriana kuhusu waliopewa ubunge, uwakilishi na udiwani kama waende kula kiapo au la.”- Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Seif Sharif Hamad.

Rais wa Serikali ya Zanzibar na Mwenyekiti wa wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein alisema aliwaandikia barua chama cha ACT wazalendo kupeleka jina la Makamu wa Rais kama Katiba inavyotaka lakini bado hawajapeleka. Alisesema nafasi mbili za Mawaziri alizoziacha wazi ni kwaajili ya ACT-Wazalendo kama chama hicho kitakuwa tayari.

NABII BUSHIRI, UTAJIRI WA KUTISHA, MALI KUSHIKILIWA, ANA NDEGE, JUMBA LA KIFAHARI, MAGARI

Soma na hizi

Tupia Comments