Top Stories

Maambukizi mapya ya corona China 105

on

China imerekodi visa vipya 105 vya maambukizi ya virusi vya Corona vilivyothibitishwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, rekodi ya kila siku kwa kipindi cha miezi mitatu na nusu, mamlaka ya afya nchini humo imesema.

Kati ya kesi hizi mpya, 96 zimeripotiwa katika Mkoa wa Xinjiang magharibi mwa nchi, ambapo kumezuka maambukizi mapya , Tume ya Kitaifa ya Afya imeripoti nchini humo.

Kesi moja imethibitishwa Beijing, tume hiyo imebaini katika taarifa yake ya kila siku kuhusu janga la Covid-19.

Kulingana na takwimu rasmi, kesi 84,165 za maambukizi zimethibitishwa katika China Bara tangu kuzuka kwa janga hilo, ambalo limesababisha vifo vya watu 4,634 nchini kote, hakuna vifo vipya vilivyoripotiwa leo Alhamisi.

MAGUFULI AWAACHA HOI VIONGOZI MSIBANI WAKIWA NA MAJONZI KUHUSU ATAKAPOZIKWA MWINYI

Soma na hizi

Tupia Comments