Shirika la Afya Ulimwenguni limesema kesi za mpox katika eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo aina mpya na ya kuambukiza zaidi iligunduliwa kwa mara ya kwanza inaonekana “kudumaa,” hata kama virusi vinaendelea kuongezeka katika mikoa mingine ya nchi, na pia Burundi na Uganda.
Katika ripoti ya Jumatatu, shirika la afya la Umoja wa Mataifa lilisema idadi ya maambukizi ya mpox “inaonyesha hali ya kuongezeka kwa jumla” lakini kwamba inaweza kuwa imeenea katika Kivu Kusini, ambapo aina ya kuambukiza zaidi ya mpox iligunduliwa kuenea mapema mwaka huu katika mji wa uchimbaji dhahabu wa Kamituga.
WHO ilikubali, hata hivyo, kwamba upimaji bado haujaenea, na kuifanya kuwa ngumu kuelewa ni jinsi gani virusi vinasamabaa.
Kulingana na takwimu za wiki iliyopita, DR Congo iliripoti chini ya maambukizi 100 zilizothibitishwa kimaabara, kutoka karibu 400 mwezi Julai.
Katika wiki za hivi majuzi, wataalam wanasema kwamba maambukizi yanaonekana kudhibitiwa, na kutoa nafasi kwa mamlaka ya afya kumaliza milipuko hiyo.
Hadi sasa, takriban watu 50,000 nchini DR Congo wamechanjwa dhidi ya mpox; Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vinakadiria kuwa chanjo milioni 3 zinahitajika kukomesha mlipuko huo.
Wiki iliyopita, mkurugenzi wa Afrika CDC Dk Jean Kaseya alisema bara hilo “bado liko katika hatua kali” ya janga la mpox, na nchi 19 zimeathiriwa. Alionya kwamba bila rasilimali zaidi kukomesha virusi barani Afrika, inaweza kuwa tishio la ulimwengu.