Kamati ya Bunge ya masula ya UKIMWI imebaini kuwa kiwango cha maambukizi ya virusi vya UKIMWI VVU kimeshuka kutoka asilimia 7 mwaka 2003/04 hadi kufikia asilimia 4.7 mwaka 2016/17.
Kiwango cha maambukizi kwa Wanawake ni kikubwa (asilimia 6.3) ikilinganishwa na Wanaume (asilimia 3.4) na kushuka kwa kiwango cha maambukizi ya VVU, Matokeo ya tisini tatu (90, 90, 90) kwa mwaka 2020 ilikadiriwa kuwa Tanzania ina Watu 1,700,000 wanaoishi na Virusi vya UKIMWI.
Imeelezwa kwamba mpaka mwisho wa robo ya Oktoba – Desemba 2020, WAVIU milioni 1.4 sawa na asilimia 83 ya WAVIU wote walikuwa wanatambua hali zao za VVU ambapo WAVIU milioni 1.36 sawa na 98% walikuwa kwenye tiba na matunzo ya ARV na 92% ya waliokuwa kwenye tiba ya ARV walikuwa na kiwango cha chini cha VVU mwilini.
KIRUSI KIPYA CHA UKIMWI KIMEGUNDULIKA , RIPOTI “TAYARI KIMEWAPATA WATU 109”