Michezo

Maamuzi ya mashabiki wa Malmo Sweden, baada ya kusikia Zlatan kanunua timu pinzani

on

Mshambuliaji wa zamani wa timu za FC Barcelona, Inter Milan na LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic amekuwa gumzo mitandaoni kufuatia mapokeo ya uamuzi wake wa kununua asilimia 50 ya hisa za timu ya Hammarby inayoshiriki Ligi Kuu Sweden.

Zlatan akiwa na jezi ya club aliyoinunua Hammarby

Kufuatia maamuzi hayo wakati huu Zlatan akiwa kamaliza mkataba wake na club ya LA Galaxy ya Marekani, mashabiki wa timu yake iliyomuibua utotoni nchini kwao Sweden club ya Malmo wameamua kuchoma moto sanamu yake iliyokuwa imejengwa nje ya uwanja wa Malmo kwa heshima na kumuenzi mchezaji huyo.

Mashabiki hao wanamuona Zlatan ni kama msaliti kwenda kununua club pinzani, kwa Malmo iliyomubua na kumpa heshim na Malmo katika Ligi Kuu ya Sweden, hata hivyo timu ya Hammarby na LA Galaxy zote zilikuwa chini ya  umiliki wa kampuni ya AEG Sweden kabla ya Zlatan kunua hisa Hammarby.

Soma na hizi

Tupia Comments