Kliniko ya kwanza ya kisasa ya meno na kinywa imezinduliwaleo jijini Dar es Salaam ili kutoa suluhisho la kudumu la matatizo ya meno nchini.
Kliiniki hiyo ya kipekee inayojulikana kama AFYA BORA COMPLETE DENTISTRY LTD inalenga kuimarisha hudumaza kinga ya meno. Hiki kitakuwa kituo cha kwanza kabisa kutoahuduma ya aina hii kikamilifu.
Mtendaji Mkuuu wa Kliniki hiyo, Dk. Donna Williams Ngirwaanasema kituo hki kitajikita zaidi katika kueneza elimu kuhusuuhusiano uliopo kati ya afya ya kinywa na afya ya binadamukwa ujumla.
“Utafiti unaonyesha kuwa magonjwa mengi yakiwemos hambulio la moyo, kisukari, kiharusi, maambukizi katika mapafu na magonjwa mengine yana mahusiano ya karibu na maambukizi yaliyopo katika kinywa,” anasisitiza na kuongezakuwa elimu hii nimuhimu iwafikie wananchi.
Dk. Williams Ngirwa amekuwa akishughulika na huduma zameno jijini Mwanza tangu akiwa mdogo na pia ana ofisiinayotoa huduma za afya ya meno nchini Marekani.
Aliwahi kuishi Mwanza mwanzoni mwa miaka ya 1970 nakujifunza mambo mengi kuhusiana na huduma hii jambo ambalolilimshawishi kuanzisha huduma hii yeye na mume wake.
Kwa mujibu wa Dk. Gilbert Tarimo ambaye ndiye daktaribingwa katika kituo cha huduma ya meno na kinywa cha AfyaBora, lengo ni kuifanya huduma ya afya ya kinywa kuwa yakinga zaidi badala ya tiba.
“Tunafanya uchunguzi wa afya ya kinywa na mgonjwa anapewaripoti ya kila kitu kuhusu kinywa chake na hatua anazopaswakuchukua ili kuboresha afya yake zaidi,” anasema
Dk. Williams Ngirwa anasema watu wengi wanaishi vizuri kwakula chakula kizuri na kufanya mazoezi lakini wanakosa afya yakinywa, pengo ambalo Afya Bora ya Kinywa wanaamuakuliziba.
Kituo hicho kilichoko mtaa wa Regent Estate jijini Dar esSalaam kinatoa huduma zote za meno ikiwemo usafishaji wameno, kuweka meno ya bandia, mpangilio wa meno na hudumanyinginezo za tiba ya meno.
Dk. Williams Ngirwa anasema watatoa fursa kwa wahitimu waelimu ya juu kikiwemo Chuo Kikuu cha Afya ya SayansiShirikishi cha Muhimbili (MUHAS) kujifunza na kuimarishafani ya udaktari wa meno.
Vilevile tangu mwezi Januari mwaka huu watoa huduma ya tibaya meno wa hapa nchini wamekuwa wakishiriki mafunzokuwawezesha kutoa huduma za kipekee na kuwawezeshamadaktari bingwa wa meno ambao hawawezi kumudukuanzisha kliniki zao binafsi, kufanya kazi katika kituo hicho.
Dk. Williams-Ngirwa amesema kwa vile watu hawana bima yameno, mpango wa Afya Bora ya Meno utatoa huduma bure zauchunguzi wa meno, usafishaji wa meno, vipimo vya x-ray, napunguzo la asilimia 20 kwa tiba kamili ya meno.
Lengo kuu la Afya Bora ya Meno na Kinywa ni kuwajengawananchi wawe na utamaduni wa kuthamini afya ya meno nakinywa ili kuboresha maisha yao.