Mabadiliko ya Tabia ya Nchi yametajwa kuwa Moja ya mambo yanayochangia Umasikini kwa jamii zilizopo pembezoni ikiwemo za kifugaji za Wamaasai hali ambayo indhoofisha ustawi wa maisha ya wananchi wa maeneo hayo.
Hali hiyo huathiri Maendeleo kuanzia ngazi ya Familia kutokana na utegemezi wao mkubwa kuwa kwenye mifugo na kilimo ambayo huathiriwa na ukame.
Akizungumza wakati akizindua mfuko utakaowasaidia kuunganisha wananchi wa pembezoni kuleta Maendeleo (ERETO SOLIDARITY FUND) mkuu wa wilaya ya Monduli Festo Kiswaga amesema mfuko huu utakwenda kuleta faraja katika jamii kwani utawasadia wananchi wa maeneo hayo kuja na miradi mbadala na hivyo kujikwamua kiuchumi.
“Hii itakua njia Moja itakayosaidia kupunguza migogoro katika umoja wa wafugaji na kuunganisha kwa jamii zote na kuondokana na utegemezi na kuleta Maendeleo kwa kasi katika jamii za pembezoni alisema Mkuu wa wilaya”
Kwa upande wake Mratibu wa Mfuko wa umoja ERETO SOLIDARITY FUND ANNA Ndiko, amesema mfuko huu unalenga kuunganisha jamii za pembezoni za Afrika mashariki ikiwemo wafugaji, Waokota matunda na jamii za warinaji asali pamoja na wahazabe ili waweze kufanya miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kudumisha matakwa Yao.
“Jamii za pembezoni ndio wanaibua miradi na kuiendesha miradi kwa kuisimamia badala ya kupokea fedha za Maendeleo na wataboresha ili kuleta suluhisho la muda mfupi.Alisema Mratibu Anna Ndiko”
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa mfuko huo Mkurugenzi wa Shirika
SHIRIKA la PWC Pastoral Women Council Maanda Ngoitiko amesema kwa niaba ya mashika wameishukuru serikali namna ya walivyowaunga mkono katika kuwasaidia wananchi kuwafikishia huduma Bora
Akiongea kwa niaba ya wananchi wa eneo hilo kiongozi wa kimila ya jamii ya wamasai amesema mfuko huo utasaidia wananchi katika kuboresha Maendeleo ikiwemo barabara, AFYA miundombinu ya barabara na maji kwasababu maeneo mengi ya pembezoni hayana uhakika wa huduma hizo.
kampeni na harembee ya mfuko huu inafanywa na Mashirika matano yakiongozwa na Shirika la Pastoral Women Council PWC ambapo zoezi hilo limefanyika makuyuni na kuhudhuriwa na wananchi zaidi ya elfu 2 wa jamii za pembezoni.