Baada ya uwepo wa malalamiko ya Vifurushi kutoka kwa watumiaji wa Simu, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepitisha mabadiliko ya kanuni ndogo za Vifurushi ikiwemo mteja kuhamisha uniti za kifurushi kwenda kwa mtu mwingine.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Eng. James Kilaba amesema dhumuni la juhudi hizo ni kupunguza tofauti kubwa iliyokuwepo kati ya bei ya Vifurushi na bei za kutumia huduma bila kujiunga na Vifurushi.
Miongoni mwa Kanuni ndogo zilizobadilishwa ni kwamba mtoa huduma hatatoa huduma za Vifurushi bila kibali cha Mamlaka.
Mtoa huduma atatoa taarifa kila wakati matumizi ya kifurushi yatakapofikia asilimia 75 na 100 kwa Vifurushi vya muda wa maongezi Data na SMS.
“Mtoa huduma ataweka utaratibu au mfumo wa kumwezesha mtumiaji wa huduma kuhamisha uniti za kifurushi kwenda kwa mtumiaji mwingine ndani ya mtandao wake kwa masharti ya kiasi cha chini kuhamisha kutakuwa 250Mb,” Kilaba
“Mtoa huduma ataweka utaratibu wa kumwezesha aliyejiunga na kifurushi chochote kuendelea kutumia muda au uniti za kifurushi ambazo zitakuwa zimesalia ndani ya muda wa matumizi uliowekwa kwa kununua tena kifurushi hicho hicho kabla ya kumalizika kwa muda wake,” Kilaba