Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) inautaarifu umma kuwa imesitisha leseni za usafirishaji abiria kwa mabasi 22 kwa kipindi cha mwezi Januari hadi February, 2023.
Akizungumza na Waandishi wa habari Johansen Kahatano Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Barabara amesema hatua hi ni kutokana na vitendo vya kuingilia Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS) na kusababisha mfumo kutotuma taarifa ama kutuma taarifa kwa kurukaruka (skipping).
“Hapa kuna baadhi ya mabasi ambayo baada ya wataalamu wa Mamlaka kufanya chunguzi, waligundua betri za vifaa vya kufuatilia mwenendo wa mabasi (VTDs) zimeharibiwa na mfumo wa umeme kubadilishwa” Kahatano