Mamlaka ya Dawa na Chakula Zanzibar ZFDA imefanikiwa kukamata mabegi manne yenye Dawa za Matumizi ya Binadamu ambazo zinadaiwa kua sio salama kwa matumizi ya Binadamu dawa ambazo zimeingia kupitia uwanja wa ndege wa Abeid Amaan karume Airport (AAKIA) siku ya Jana
Kaimu Mkurugenzi wa ZFDA amesema dawa hizo zimeingia kupitia ndege ya Ethiopia Airline zikitokea Nchini India ambazo zimekosa kibali cha Uingiaji na baada ya Mamlaka hiyo kukagua na kugundua dawa hizo hazitambuliki kwa uingiaji nchini Zanzibar ,kati ya Dawa hizo zilizokutikana ni Dawa za Antibayotiki ,Dawa za Kensa Nk.
Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Sabrina Idrisa Ahmada amebainisha kua mzigo huo ulipokelewa na Wakala uwanja wa ndege Nassor na alipoulizwa alijibu hana maelezo ya kutosha kuhusu mzigo ambao kwa sasa umeshikiliwa