Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba Amezitaka Benki zote Nchini kuweka mazingira wezeshi ya Mikopo na Riba nafuu kwa Wananchi ili kuondokana na mikopo ya Kausha damu.
Ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la CRDB Lililopo katika Halmashauri ya wilaya ya kilolo, Mji mdogo wa Ilula.
Mhe.Serukamba amesema kuwa Benki zinaweza kuweka utaratibu wa upatikanaji wa mkopo kwa muda mfupi ili kutatua changamoto kwa Wafanyabiashara kuondokana na mikopo ya kausha damu inayowatesa wananchi wengi katika kipindi hiki,
Aidha Mhe. Serukamba amewataka wafanyakazi wa CRDB kubuni mikakati ya utoaji Elimu kwa Wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia huduma za Benki.
Mhe. Serukamba ametoa wito kwa Watanzania kujenga tabia ya kuweka akiba kwenye Benki pamoja na kutumia Huduma za Benki.
Hata hivyo Mhe. Serukamba amemaliza kwa kuipongeza benki ya CRDB kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kufikisha huduma nzuri kwa Wananchi na kuwataka kuongeza juhudi ili Benki hiyo iwe mfano wa mafanikio ya kitaasisi huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwa pamoja nao katika kila hali.