Katika jitihada za kuboresha upatikanaji wa haki kisheria, Mahakama imefanya maboresho ya kanuni ambazo zimerahisisha mchakato wa kupata haki kwa wananchi, hususan kwa wajasiriamali wadogo. Maboresho haya yanapanua wigo wa wasuluhishi na kupunguza gharama za mashauri, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa haki kwa makundi yote.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Kituo cha Huduma za Haki Mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Mashauri, Desdery Kamugisha, alisema kuwa maboresho haya yanajibu mahitaji ya wananchi kwa kurahisisha mchakato wa kushughulikia migogoro na kutoa suluhu kwa haraka zaidi.
Naye Maira Kasonde, Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Huduma za Kimahakama, alisema kuwa kituo hiki kinaongeza uwajibikaji wa mahakama kwa kusikiliza malalamiko ya wananchi, kujitathmini na kuboresha huduma zinazotolewa.
katika maboresho ya sheria na kanuni za ufunguaji wa mashauri na kusikiliza mashtaka kwa njia ya mtandao, mahakama imeboresha utoaji wa maelezo ya mshtakiwa katika kituo cha polisi kwa njia ya video na sauti ili kuweka uwazi katika utoaji wa maelezo ya kesi husika
Mwaka 2022 mahakama ikaanzisha kituo cha huduma kwa wateja hali iliyochangia wananchi kuwa na imani na mahakama kwa kutoa malalamiko kuhusu huduma za kimahakama
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wanaopata huduma za kimahakama wamesema kuwa huduma hii imeongeza ufanisi wa utoaji haki na kuwahamasisha watumishi kufanya kazi kwa haraka, kwani upatikanaji wa haki ni msingi muhimu katika jamii.