Habari za Mastaa

Hussein Machozi amezungumzia changamoto anazokutana nazo Italia

on

Mwanamuzi staa wa Tanzania ambaye aliwahi kutamba miaka ya nyuma Hussein Machozi ambaye alikuwa kimya muda mrefu amesema anakutana na changamoto nchini Italia anakofanyia kazi za kimuziki kwa sababu hakuna studio nyingi.

Akizungumza kwenye Leo Tena ya Clouds FM kuhusu studio na namna anavyofanya kazi akiwa Italia Hussein Machozi amesema: 

“Italia kuna changamoto za studio, kuzalisha ni gharama. Kuna usimamizi mkubwa kwenye suala la kulinda ubora wa kazi za wasanii. Huu wimbo niliurekodi papa hapa. Nilipokwenda nje nilibeba kazi zangu zote ila director aliipenda hii ifanyiwe video.” –  Hussein Machozi.

Mbali na kueleza juu ya changamoto za studio na mazingira ya kazi nchini Italia, Hussein Machozi ameeleza pia sababu za kuja Tanzania licha ya kuishi Italia akisema:

“Nimekuja home kwa ajili ya likizo. Mimi ndiye baba wa mama yangu; mimi ndiyo baba wa mwanangu nimekuja kuwasalimu. Familia yangu na mtoto wangu wapo Mwanza. Siwezi kuwatenga nitakuwa narudi kuwasalimu.” – Hussein Machozi.

Mrisho Mpoto kaongea baada ya kutukanwa kumuunga mkono Rais Magufuli

Soma na hizi

Tupia Comments