Jopo la madaktari 24 kutoka Korea Kaskazini leo July 2 2022 wamewasili nchini na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ambapo wataelekea katika Jimbo la Buchosa, Sengerema jijini Mwanza ambapo watatoa huduma mbalimbali za kitabibu kwa wakazi wa maeneo hayo.
Ujio wa madaktari hao nchini umekuja kutokana na jitihada za Mbunge wa Buchoasa Eric Shigongo, akizungumza wakati wa mapokezi, Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo amewashukuru madaktari hao kwa kuja nchini kwa kujitolea kuwasaidia wananchi wa Buchosa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya bure na wataanza kutoa huduma kuanzia July 4 2022.
Shigongo amesema huduma za kitatibu zitaanza Jumatatu ya July 4 2022 na kuwasihi wananchi wenye matatizo mbalimbali, kujitokeza kwa wingi kupata huduma za kitabibu kutoka kwa madaktari hao bure.
Kwa upande wake, kiongozi wa msafara huo, Dr. Bae amesema anajisikia furaha kufika Tanzania ambapo yeye na wenzake wapo tayari kuwapa huduma za kitabibu wananchi waliopo katika visiwa kadhaa vya Ziwa la Victoria pamoja na maeneo mengine na kueleza kwamba wamekuwa na utaratibu wa kuja nchini kila mwaka.