Madaktari katika hospitali za serikali katika majimbo kadhaa ya India wamegoma na kuanzisha maandamano leo Jumatatu, Agosti 12, 2024 baada ya ubakaji na mauaji ya daktari mwanafunzi huko Kolkata siku ya Ijumaa, Agosti 09, 2024.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31 alivamiwa katika chuo cha serikali cha RG Kar, ambapo alikuwa akifanya kazi, alipokua amepumzika katika chumba cha semina baada ya kula chakula cha jioni na wenzake.
Mwili wake ulipatikana ukiwa na majeraha mengi na uchunguzi wa maiti umethibitisha kuwa alifanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na kuuawa, polisi walimkamata Sanjay Roy, “mhudumu wa kujitolea” katika hospitali hiyo, akihusishwa na shambulio hilo.
Majukumu ya Roy hayakuwa wazi lakini ripoti za vyombo vya habari vya ndani zinasema kuwa alikua akifanya kazi katika hospitali hiyo kama dalali, na kusaidia kuongeza idadi ya kulazwa kwa wagonjwa kwa malipo ya pesa.
Maandamano ya madaktari wanaodai haki na usalama bora mahali pa kazi ambayo yalianza tangu leo asubuhi huko Kolkata, magharibi mwa Bengal, sasa yameenea