Madaktari wa Shenzen, China mwaka 2019 walifanya uchunguzi wa dharura wa kutoa kijiko cha chuma chenye urefu wa sentimita 13 baada ya kukimeza kwa bahati mbaya wakati akijaribu kutoa mfupa wa samaki kwenye koo lake.
Mgonjwa huyo aliyefahamika kwa jina la Lily, aliripotiwa kumeza kijiko kabla ya kwenda kulitazama Tamasha la Qingming mnamo Aprili 5, lakini hakujisumbua kwenda hospitali hadi siku nne baadaye, kwa sababu hakusikia maumivu yoyote tumboni mwake.
Hatimaye alipofika katika Hospitali ya Shenzhen Nanshan kuwaeleza madaktari wa hapo kilichotokea, waliagiza kupigwa picha ya X-ray na kuona kijiko kikubwa cha chuma kikiwa kimekwama kwenye utumbo wake.
“Kwa vile kijiko kilikuwa katika nafasi ya mlalo, tulikirekebisha kwa uangalifu kabla ya kukitoa nje kwa wima,” Dk Sun Tingji aliiambia Pear Video. Kijiko cha chuma kilikuwa kimesababisha uvimbe na lakini madaktari waliweza kukiondoa, na kufuatia matibabu, mwanamke huyo aliruhusiwa na alipona kabisa