Michezo

Madee amuita mwanae jina la Mesut Ozil wa Arsenal

on

Msanii wa Bongofleva Madee leo kupitia Instagram account ya mtoto wake Chonge imethibitisha kuwa amepata mtoto wa kiume na mpenzi wake Mima na kumpa jina la kiungo wa Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil.

Madee ambaye ni shabiki wa Arsenal mtoto wake wa kiume aliyezaliwa November 4 2020 amempa jina la Ozil, huyu akiwa ni mtoto wa tatu wa Madee baada ya wasichana Saida na Chonge.

Kwa sasa Mesut Ozil ambaye ndio mchezaji anayelipwa zaidi katika kikosi cha Arsenal, ameondolewa katika Vikosi vya Arsenal na kufanya mazoezi na team B.

Soma na hizi

Tupia Comments