Habari za Mastaa

Madee atinga Kariakoo kukamata bidhaa zenye logo feki ya Dogo Janja ( + Video)

on

Murch 17 mwaka huu Msanii wa bongo Fleva Madee  alichukua uwamuzi wa kutinga mitaa ya kariakoo kukamata bidhaa zenye logo feki ya Dogo Janja.

Madee ambaye aliongozana na Polisi Pamoja na management yake walifika mitaa ya Kariakoo na kukamata wauzaji wa Duka moja ambao waliwakuta na bidhaa hizo zenye logo ya Dogo Janja

Hata hivyo AyoTV ilikuepo eneo la tukio na alipojaribu kutaka kuzungumza na wahusika akiwemo mtuhumiwa na Msanii Madee ilishindikana kwani Tayari swala lilikuwa lipo chini ya polisi na walikuwa wakishughulikia Sakata Hilo.

Hata hivyo watuhumiwa walifikishwa polisi ambapo Dogo Janja pia alifik na aliahidi kuzungumzia swala hilo hivi karibuni baada ya taratibu walizozifuata kukamilika.

PLAY hapa chini kwa taarifa kamili

VIDEO: SWALA LA MZEE YUSUPH KURUDI KWENYE MUZIKI, ALIYEZAA NA HAMMER Q KAZUNGUMZA 

Soma na hizi

Tupia Comments