Michezo

Madee kafunguka baada ya kupewa zawadi ya jezi na Saido Ntibazonkiza

on

NI Headlines za Yanga SC ambayo jana ilipata ushindi wa penati 4-3 katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi 2021 visiwani Zanzibar dhidi ya wapinzani wao wakuu Simba FC, Sasa miongoni mwa mastaa waliofika uwanjani hapo na kushuhudia mtanange huo ni mkali kutokea Bongo Flevani Madee.

Madee alipewa jezi ya Yanga na mchezaji aliechezea namba 60 aitwae Ntibazonkiza, Madee akizungumza na Ayo TV & Millardayo.com alisema ‘NI Kati ya Wachezaji ninaowapenda sana Saido na wakati nimefunga Safari kutoka Dar kuja Zanzibar niliwauliza watu vipi  Ntibazonkiza atakuwepo uwanjani nikaambia ndio sikutegemeana huenda labda alipata taarifa zangu kuwa namkubali na ndio akanifuata na kunikabidhi hii jezi yake aliyoicheza katika mechi dhidi ya Simba’- Madee

Ubingwa huu ni mkubwa nawaambia hivi safari hifi tumeamua sana sana ningependa kumwambia Ommy Dimpoz pole kwa matokea hayo na hii ndio Yanga’- Madee

KAULI YA SAIDO NTIBAZONKIZA AKIFUNGA PENATI YA USHINDI KWA YANGA NA KUMFUATA MADEE

KAULI ZA NIYONZIMA, WAZIRI JR NA MAKAPU BAADA YA UBINGWA WA YANGA DHIDI YA SIMBA

Tupia Comments