Habari za Mastaa

Baada ya kuenguliwa kwa ‘tema mate’ kwenye tuzo za KILI, Madee amezungumza haya

By

on

Screen Shot 2014-03-25 at 8.51.46 PMMsanii Madee toka Tip Top Connection ni miongoni mwa wasanii ambao hawajaingizwa kwenye kushindania tuzo muziki Tanzania (KTMA) 2013/2014 baada ya baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kutangaza kwamba ‘tema mate tuwachape’ ya Madee, ‘nimevurugwa’ ya Snura na ‘uzuri wako’ ya Jux zimetolewa kutokana na video zake kukosa maadili.

Baada ya hapo millardayo.com na AyoTV zilimfata Madee aliekubali kuzungumza Exclusive kwa kusema >>’Kikawaida lazima utashtuka lakini ndiyo tayari maamuzi yameshafanyika na hao walioamua wameshaamua kwa hiyo hakuna tatizo maisha yanaendelea, ‘tema mate tuwachape’ mimi nilipataga taarifa tu kuwa video ina matatizo inafungiwa sijui nini’

‘Nilitarajia kuletewa barua rasmi kuwa video yako imefungiwa mwisho wa siku leo napata taarifa kuwa wimbo wako umetolewa kwa sababu hauna maadili, siwezi kuvunjika moyo manake hata mwaka mmoja mi kila siku nafanya kazi si kwa sababu ya tuzo za Kili, hii sio mara ya kwanza kushiriki kwenye Kili Music kisha kutoka bila kupata kitu chochote sijawahi kuvunjika moyo hata siku moja’ – Madee

‘Umewaambia Wananchi wachague ngoma zilizofanya vizuri mwaka jana na katika zilizofanya vizuri mwaka jana ndio hizo pia za Madee, ingekua vizuri kama wangeorodhesha nyimbo ambazo hazitakiwi kupigiwa kura…….. mwananchi katumia hela yake kunipigia kura halafu mwisho wa siku unamwambia wimbo fulani haupo kwa sababu za kimaadili, ataona kama umemtapeli au umemdhulumu wakati ujao anaweza asifanye hivyo tena’

Ili kuwa na uhakika wa kupata kila stori inayoifikia millardayo.com karibu ujiunge na mimi mtu wangu kwenye twitter facebook na instagram kwa jina hilohilo la @millardayo

Tupia Comments