Madereva pikipiki maarufu bodaboda Mkoani Kigoma wamelazimika kuandamana na kufunga barabara katika eneo la Mwanga Kigoma Ujiji kwa madai ya Jeshi la Polisi kutumia nguvu kuwakamata lakini pia wakiwatuhumu baadhi ya askari kuchukua fedha bila ya makosa yoyote ambapo bodaboda wanadai kua ni manyanyaso kwao.
Leo 09 January 2025 ni siku iliyoanza kwa utulivu lakini ghafla majira ya sa tano asubuhi kundi la dereva Bodaboda lilivamia katika Ofisi za Mkuu wa mkoa Kigoma wakipiga kelele kudai haki lakini baada ya kubaini kuwa Mkuu wa mkoa Thobias Andengenye hayupo,maandamano hayo yakahamia eneo la Round about ya Samaki Mwanga ambapo walifunga barabara ikiwa ni sehemu ya kufikisha ujumbe wao kwa serikali wakisema wameshoshwa na manyanyaso.
Wakizungumza na Ripota wa @ayotv Kigoma madereva hao wanaeleza sababu zilizowafanya kuingia barabarani kudai haki zao,ambapo wakati vurugu hizo zikiendelea Jeshi la polisi liliifka na kulazimika kutumia mabomu ya machozi na virungu kuwatanyisha waandamanaji katika eno hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoani wa Kigoma SACP Filemon Makungu ameeleza kutofahamu sababu ya maandamano hayo lakini amedai wengi wao kutofuata sheria na kukosa baadhi ya nakala muhimu wanapokua barabarani wakifany huduma za usafirishaji.
Tangu kuanza kwa mwezi Dismember mwaka 2024 Jeshi la Polisi mkoani Kigoma lilianza kufanya operesheni ambayo pikipiki nyingi zilitiwa nguvuni kwa makosa mbalimbali na kupelekwa kituoni ambapo inakulazimu kulipa faini kwa kila kosa ulilokutwa nalo ndio unapewa pikipiki yako.