Huku maandamano yakiwa kwenye kamata kamata na sitisho nchini Kenya,kukishuhudiwa machafuko makubwa katika baadhi ya maeneo ya Kibera huku baadhi ya waandamanaji wakionekana wakikabiliana na maafisa wa GSU ambao walikuwa wakiwarushia vitoa machozi.
Barabara zote zinazoelekea Ikulu zimekuwa chini ya ulinzi mkali kuanzia mapema Jumatatu asubuhi huku viongozi na waandamanaji kadhaa pia walikamatwa kutoka pembe tofauti za mji mkuu katika juhudi za kuzuia machafuko.
Maafisa wa polisi walilazimika kuwarushia vitoa machozi waandamanaji kwa nia ya kuwatawanya.
Ukiachana na huko nchini Afrika Kusini polisi imesema kuwa imewatia nguvuni watu 87 kate nchini kuhusiana na maandamano ya upinzani.
Waziri wa polisi Bheki Cele alisema Jumatatu kuwa wengi miongoni mwa waliokamatwa Jumatatu walikuwa ni kutoka jimbo la Gauteng.
“Wengi walipatikana wakitengeneza vilipuzi vya moto, wakifunga barabara na kujaribu kuwazuia watu kwenda kazini. Hawakuandamana kwa amani ,” alisema.
Aliongeza kuwa zaidi ya magurudumu 24,000 yalikamatwa na polisi katika miji tofauti.
Alisema kuwa polisi wanashirikiana na wanajeshi kuimarisha hali ya utulivu.
Chama kikuu cha upinzani ambao ni wachache – Economic Freedom Fighters (EFF) kinaongoza kile knachoitwa ‘’kufungwa kwa shughuli za kitaifa’’. Kilianza maandamano Jumapili saa sita usiku.
EFF kinatoa wito wa kujiuzulu kwa Rais Cyril Ramaphosa na kumalizika kwa mzozo wa nishati nchini humo.
Madiwani watatu wa EFF walikuwa miongoni mwa dazeni ya watu waliokamatwa kuhusiana na vitendo vinavyozunguka kufungwa kwa kitaifa.
Msemaji wa polisi Brig Athlenda Mathe alithibitisha madiwani wa wadi za chama hicho walikamatwa Gauteng, Free State na Mpumalanga.