Michezo

Kama ulimis kipigo walichopokea Real Madrid jana – angalia magoli hapa

on

article-2739221-20F4381200000578-812_636x421Real Madrid jana usiku walikiona cha mtema kuni kwenye wiki ya pili ya ligi kuu ya Hispania baada ya kupokea kipigo kizito kutoka kwa Real Sociedad.

Real ambayo jana ilicheza bila mchezaji wake tegemeo Cristiano Ronaldo ambaye hayupo fiti ilianza mchezo kwa kasi na kuanza kupata magoli mawili ya kuongoza kupitia kwa Gareth Bale na Ramos lakini kibao kikawageukia na mpaka kufikia mapumziki matokeo yalikuwa 2-2.

Kipindi cha pili Real Sociedad walirudi kwa kasi na kufanikiwa kuongeza magoli mawili na mpaka mpira unakwisha walikuwa wameshinda 4-2 dhidi ya mabingwa wa ulaya.

Angalia magoli hapa…

Real Sociedad vs Real Madrid 4-2 HD – All Goals… by bbdtivi

Tupia Comments