Michezo

Rais wa klabu ya Real Madrid ya Hispania kafanya hili kwa wakimbizi hawa kutokea Syria (+Pichaz)

on

Rais wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Florentino Perez ambaye amezoeleka kuingia katika headlines kwa masuala yake ya kufanya usajili mkubwa kwa wachezaji ambao klabu yake inawahitaji, huenda umezoea kumsikia katika suala hilo, safari hii kafanya hili kwa wakimbizi kutokea Syria.

real-madrid-syria-_3444522b (1)

Florentino Perez ameingia katika headlines baada ya kuwapa nafasi wakimbizi kutoka Syria kutembelea uwanja wa klabu ya Real Madrid Santiago Bernabeu pamoja na kuwapa mualiko wa kuhudhuria mechi yao dhidi ya Granada.

syrian-refugee-rea_3444524b

Usama Alabed Almohsen na watoto wake Zied na Mohammed ndio waliyopata mualiko huo kutoka kwa Perez. Usama na familia yake waliwasili Hispania kwa usafiri wa treni usiku wa Jumatano ya September 16, hata hivyo Usama ambaye alikuwa kocha wa mpira wa miguu wakati yupo Syria amepewa nafasi ya kuongeza taaluma yake ya ukocha katika chuo cha Madrid.

Syrian-Refugees-Visit-the-Santiago-Bernabeu-Stadium

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments