Maelfu ya watu wameandamana hivi punde katika mitaa ya Ouagadougou usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano ili kuzuia uwezekano wa mapinduzi ya kijeshi nchini humo, vyanzo kadhaa vimesemaleo Jumatano
Kulikuwa na maelfu ya waandamanaji wanaodai kuwa wanaharakati na wafuasi wa utawala wa kijeshi. Walipiga kambi kwenye barabara kuu ya mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.
Maandamano kama hayo pia yameripotiwa katika miji mingine kama vile Bobo-Dioulasso na Gaoua. Wafuasi hawa wote wanadai kwamba wamesikia kuhusu uwezekano wa jaribio la mapinduzi dhidi ya Kapteni Ibrahim Traoré.
Na ili kuzuia hili, wanasema, waliingia mitaani. Kwa miezi kadhaa, wafuasi wa utawala wa kijeshi wamekuwa wakikesha kila usiku katika maeneo makubwa ya Ouagadougou.
Uvumi wa mapinduzi ya kijeshi umeongezeka hivi majuzi nchini Burkina Faso. Mwanzoni mwa mwezi wa Septemba, askari watatu – walishtakiwa na kuwekwa kizuizini kwa “njama za kijeshi, ukiukaji wa maagizo, njama dhidi ya usalama wa taifa, njama za uhalifu na kuhatarisha maisha ya wengine “, kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa kijeshi. Wote walikiri makosa yao , iliongeza mahakama hya kijeshi.