Ad

Michezo

Mafanikio ya Man City chini ya Kocha Pep Guardiola

on

Manchester City imeweka rekodi ya kuwa timu kubwa kutoka England iliyoshinda mechi nyingi mfululizo ikiwa imeshinda mechi 15, kufunga magoli 40 na kuruhusu magoli 5 huku ikiwa na ‘clean sheets’ 10 chini ya Pep Guardiola.

Kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich amefikia katikati ya Msimu wake wa Tano kama Kocha wa Manchester city. Pep Guardiola alipata ushindi wake wa 200 kama Kocha wa Manchester City siku ya Jumatano kikosi chake kilipoifunga Swansea City katika Kombe la FA.

Mabao kutoka kwa Kyle Walker, Raheem Sterling na Gabriel Jesus yalisababisha Man City kuwa salama na kujihakikishia kuingia robo fainali kwa ushindi huko Wales Kusini.

Mkatalunya huyo alichukua kazi ya kuinoa Man City mnamo mwaka 2016 kufuatia kazi nzuri aliyoifanya Barcelona na Bayern Munich. Miaka minne ya Guardiola akiwa Camp Nou aliipatia Barcelona si chini ya mataji 14, pamoja na ushindi mara mbili wa Ligi ya Mabingwa.

MREMBO MDOGO MUUZA SAMAKI, NYANYA ANAINGIZA MAMILIONI “NALIMA MPAKA NALALA SHAMBA, NIMEAJIRI”

Soma na hizi

Tupia Comments